Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Abbasi katika mkutano huo alisisitiza juu ya umuhimu wa ubunifu, mshikamano wa pamoja na kuinua uwezo binafsi wa wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Al-Mustafa, ili waweze kukabiliana ipasavyo na changamoto za zama za kisasa.
Akieleza huku akitoa shukrani kutokana na juhudi na kujitolea kwa walimu na wanaharakati wa kidini katika kuitumikia jamii na nchi, kwamba mawasilisho ya kitaaluma ya Hujjatul-Islam Nasir Damiati na Zaher Yahya yalikuwa ya thamani na yanastahili pongezi.
Rais wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa alisisitiza: Bila shaka, jukumu letu ni kuwaunga mkono wahitimu na taasisi walizozianzisha. Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, anaendeleza jukumu lake katika kuendeleza njia ya Imam Khomeini (r.a) ya kuanzisha vituo maalumu vya elimu kwa ajili ya wanafunzi wasio Wairani. Sisi tunabeba sehemu tu ya jukumu hili kubwa, na alhamdulillah hadi sasa tumeweza kuhudumia makumi ya maelfu ya wanafunzi kutoka zaidi ya nchi 120 duniani.
Rais wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa alisisitiza kuwa mfumo wa jadi wa hawza, kwa peke yake, hauwezi tena kukidhi mahitaji mbalimbali ya zama za sasa, na akasema: Hatudai kuwa kila kitu kiko kamili, lakini tumejitolea kuendeleza njia ya marekebisho na maendeleo.
Kisha akaikosoa mitazamo inayofupisha mafanikio ya wanafunzi wa hawza katika uwezo wa kufundisha tu kitabu cha Makaseb, na akabainisha: Swali ni hili: Je, uwezo wa kufundisha Makaseb peke yake unaweza kutatua matatizo yote ya binadamu? Ni kosa kuweka sehemu ndogo badala ya jumla. Hakuna mtu mmoja anaeweza kufanya kila kitu peke yake. Tunahitaji mgawanyo wa majukumu na utaalamu mbalimbali ili kila mmoja awe na mchango wenye tija katika uwanja wake.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Abbasi katika sehemu inayofuata ya hotuba yake, alisisitiza juu ya umuhimu wa matumaini na imani katika ahadi ya Mwenyezi Mungu kwamba mwishoni mwa historia, watu wema ndio watakaorithi ardhi, na akasema: Badala ya kujikita katika wingi wa mambo, ni lazima tukiweke kitovu katika ubora wa mipango.
Akaeleza kuwa ushirikiano na umoja ni ufunguo wa maendeleo, na akasisitiza: Ushirikiano ni mgumu zaidi kuliko kazi ya mtu mmoja; kwani unahitaji subira na kuvumiliana. Hatupaswi kwa sababu ya kutofautiana kimtazamo au kukataliwa kwa pendekezo moja, kuanzisha jumuiya mpya. Kipaumbele chetu kinapaswa kuwa umoja, si mgawanyiko.
Rais wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa pia alisisitiza juu ya umuhimu wa kuinua ujuzi binafsi, na akaeleza: Kila mmoja wetu anapaswa kuongeza uwezo wake. Katika Chuo Kikuu cha Al-Mustafa, masomo mapya ya ujuzi yameanzishwa, ambapo kila mwanafunzi anaweza kuchagua kulingana na mvuto na kipaji chake.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Abbasi, katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, ambayo iliambatana na masiku ya maombolezo ya shahada ya Bibi Fatima Zahra (s.a), alitoa pole kutokana na msiba huu mkubwa, na kuwaomba wote waliohudhuria waeneze uzuri wa maneno na mafundisho ya Ahlul-Bayt (a.s) katika jamii.
Rais wa Al-Mustafa, akiwaambia mahsusi wahitimu wa Indonesia, aliwashauri: Mtakutana na changamoto na upinzani ambao huenda marafiki zenu walioko Iran hawajawahi kuukutana. Msikate tamaa. Kwa kushauriana pamoja na kazi ya pamoja, tafuteni njia mpya za ajira na shughuli katika nyanja mbalimbali.
Chanzo: https://news.miu.ac.ir/?p=47933
Maoni yako